ads

Kiungo Philippe Coutinho ameomba kuondoka Liverpool" ili kutimiza ndoto yake ya kuhamia Barcelona kwa mujibu wa taarifa.


Kiungo huyo Mbrazili amekuwa akihusishwa na kutaka kujiunga na miamba hiyo ya Catalans tangu mwanzo wa msimu huu.

Lakini Liverpool chini ya kocha Jurgen Klopp wamesisitiza kuwa kiungo huyo mwenye miaka 25 hatoondoka msimu huu.

Gazeti la Mundo Deportivo limeripoti kuwa Barcelona imekuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na Liverpool wakati kiungo huyo kiendelea kuomba kuondoka.

Miamba hiyo ya Hispania imeongeza presha ya kumtaka mchezaji huyo katika usajili wa dirisha dogo mwezi ujao.

Wakati Coutinho akiaminika kuwa ndiyo chaguo la kwanza la kocha wa Barca, Ernesto Valverde, gazeti la SunSport limeripoti kuwa miamba hiyo ya Hispania wanaweza kugeukia kwa kiungo wa Arsenal, Mesut Ozil kama wakishindwa kumnasa Coutimho.

Coutinho alitaka kuhamia Hispania mwanzo wa msimu huu baada ua miamba hiyo ya Catalan kuuza Neymar kwa Paris Saint-Germain kwa uhamisho uliovunja rekodi wa pauni 200 milioni.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: