Simba ipo Afrika Kusini, kujiandaa na msimu mpya wa mwaka 2017/18 lakini hali ya hewa ya huko ni ya baridi kama wachezaji wanavyokiri na kuifurahia kwamba imewawezesha kufanya mazoezi kwa muda mrefu.
Yusuph Mlipili ni beki mpya wa Simba ambaye ameanza kula matunda ya timu hiyo kwa kusafiri kwenda nje ya nchi, amekiri kwamba kuna baridi kali, lakini linawasaidia kufanya mazoezi kwa muda mrefu kwa ajili ya pumzi.
"Ni baridi ili tunafurahia kwani mazoezi tunafanya kwa muda mrefu bila kuchoka, naamini yatatufanya tuwe fiti tayari kwa kazi ya msimu unaokuja," alisema.
Naye kiungo wa timu hiyo, Mzamiru Yasini alisema wanafurahia kambi waliyoweka nchini humo kwani inawafanya kuwa watulivu na kujijenga kisaikolojia kwa kazi iliyo mbele yao.
"Tunajipanga kwani tunajua ushindani utakaokuwepo dhidi ya wapinzani wetu, naamini tutarejea na kitu kipya zaidi," alisema.
Post A Comment: