
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Ruyagwa Kabwe amefunguka na kumshauri Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kuwa anapaswa kuwa na msimamo katika kuisimamia serikali kama alivyofanya jana na kudai hii itamfanya aweke 'legacy'.
Zitto Kabwe amesema hayo baada ya juzi Mei 8, 2018 Spika wa Bunge kumtaka Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage kuja na maelezo ya kutosha kuhusu tatizo la sukari na mafuta nchini baada ya kutoridhishwa na majibu ya waziri huyo bungeni na kusisitiza kuwa haiwezekani wananchi wakawa wanaumia kwa gharama kubwa ya bidhaa hizo.
"Namna ambavyo Spika Ndugai amesimamia suala la majibu ya Serikali kuhusu kadhia ya Sukari na Mafuta ya Uto (kula) inanikumbusha bunge la tisa. Ndugai sasa ameanza kuweka βlegacyβ yake. Aendelee hivi hivi ila jambo la muhimu zaidi suala la mafuta litazamwe kwa muktadha wa Wakulima wa Mawese na Alizeti" alisisitiza Zitto Kabwe
Kutokana na Spika wa Bunge na bunge kiujumla kutoridhika na majibu ya Waziri Mwijage hivyo spika wa bunge Job Ndugai aliomba maelezo zaidi na kutaka swali hilo kuulizwa tena wiki ijayo ili serikali ije na majibu ya kueleweka na yenye tija.
Post A Comment: