Je unahitaji mkopo?, waombaji wengi wa mikopo ya benki hukataliwa kupewa kutokana na kutokua na uelewa wa mabenki yanaitaji nini na sifa gani!, na hii inatokana na kutokujua mapema sifa ambazo benki huangalia kabla ya kutoa mikopo, japo masharti hutofautiana toka benki hadi benki ila sifa zinazoangaliwa wakati wa ukopaji zinafanana kwa benki zote.
Zifuatazo ni sifa muhimu ambazo ni lazima kuwa nazo ili kupata mkopo kupitia benki yeyote ile...
Je wewe ni mteja mpya au wazamani katika benki husika?
Ili upate mkopo, taasisi au benki itahitaji kujua kumbukumbu zako za kibenki kutaka nyuma ulipoanza huduma ya kibenki, wataitaji kujua hili ili kupata picha halisi ya mzunguko wa fedha kwenye akaunti yako, hii itawapa uhakika kama wakikupatia mkopo wakupe wa shilingi ngapi na kukupangia marejesho utakayo rejesha ya mwezi yawe ya shilingi ngapi kutoka na uwezo wako wa mzunguko kifedha.
Je unabiashara unayoifanya?
Benki nyingi wanapenda kutoa mikopo kwa wafanyabiashara na wajasiriamali, kwa hiyo iwapo malengo yako yalikua ya kukopa ili ujenge ni vyema kwenye sababu ya kukopa ukatoa sababu ya kupanua mtaji wako wa biashara, wanaangalia biashara au shughuri inayozalisha kipato zaidi ili kuwa na uhakika wa marejesho ya mkopo iwapo wakikupatia, na kwenye biashara ni rahisi zaidi kurudisha pesa yao maana pesa iatakua inazunguka na kutoa faida, na lazima biashara iwe yenye mzunguko ambao unauhakika.
Je unahistoria ya ukopaji, na wapi ulitoa mtaji?
Maswali kama haya yanaulizwa ili kujua tabia yako ya kukopa na urudishaji wa pesa na kama ni msumbufu kwenye malipo au la, hili linawapa uhakika wa kukujua vizuri maana wanataka kukukopa pesa yao. Na kama ni mtaji ulianza na shilingi ngapi, hii ni ili wajue biashara yako inakuza mtaji kiasi gani, na iwapo mtaji ulionao ni wa kukopa au kupewa.
Je ni aina gani ya biashara unayoifanya?
Ni lazima watake kujua ni aina gani ya biashara unayoifanya, na lazima waje waitembelee na kuiona. Na watataka kujua mzunguko wake wa hio biashara ulionayo na inatengeneza faida kiasi gani, na kama utakua unaifanyia hesabu kila siku hii itakuweka kwenye manufaa zaidi ya kupewa mkopo, yote haya yanafanyika ili benki ijue unafaa kupewa mkopo wa kiasi gani!.
Je biashara yako inamtaji kiasi gani?
Benki lazima ijue mtaji wako ulionao na mara nyingi hawawezi kukupa pesa iliyo zaidi ya mtaji wa biashara ulionao, na hata kama wakikupatia lazima waone kwanza hesabu ya biashara yako ili kujua mzunguko ulionao kama unaweza kutosha kulipa marejesho yanayoendana na kiasi cha mkopo ulioomba, hivyo ufanya hesabu kwenye biashara unakuweka katika hali nzuri ya kupewa mkopo.
Dhamana
Benki lazima iangalie dhamana ulionayo, na sio mpaka iwe nyumba mabenki mengine wanahitaji dhamana ya vitu ulivyonavyo, hata kama ukiwa umepanga unaweza kupewa mkopo, ila kwa mfano wa vitu vya ndani wakija kuthaminisha, kama TV umeinunua kwa shilingi laki moja, kwao itakua na thamani ya elfu hamsini!, kwa hio kila kitu kitakua nusu ya thamani ulio nunulia.
Mdhamini
Mara nyingi hii inafanya kazi iwapo utakua hauna nyumba na umepanga, hivyo itakubidi umatafute mdhamini ili akudhamini na sharti atakalopewa mdhamini lazima akubali kulipa marejesho yako ya kila mwezi ya mkopo iwapo tu kama wewe yatakua yamekushinda kulipia, na ukiwa na nyumba,
nyumba yako ndo itakua mdhamini wako.
Mkataba wa pango la biashara
Iwapo hapo unapofanyia biashara ni pango ambalo umepangishwa, itabidi upeleke benki kopi ya mkataba wa hio sehemu husika na hutumika kupigia hesabu za faida yako ya mwezi ukiwa imeshatoa na kodi yako ya pango.
TIN number yako
Utahitaji uwe na tin namba yako ya kukutambulisha kama mfanyabiashara uliosajiliwa na serikali.
Mkataba wa pamgo la kuishi
Iwapo umepanga, utahitajika kupeleka na mkataba wa sehemu unayoishi.
Kitambulisho cha mpiga kura
Benki itahitaji kitambulisho chako na cha mkeo/mumeo kama umeoa/olewa ili kudhibitisha utambulisho wako na wa mwenza wako ambae atakua kama mdhamini wako.
Barua ya mwenyekiti
Benki itahitaji barua toka kwa mwenyekiti ili kuhakiki makazi unayoishi na kama hujafungu akaunti itatumika kufungulia akaunti.
Hayo ndo masharti ambayo kiumeni.com tumekuandalia na sifa mabenki yanazoitaji, zingatia na hutokosa mkopo.
Post A Comment: