.MCHAKAMCHAKA wa Ligi ya Mabingwa Ulaya unaendelea wiki huu ambapo vigogo Real Madrid, Barcelona na Manchester United watahakikisha wanapanga vikosi vya maana ili kupata tiketi yao ya kutinga hatua ya mtoano ya 16 bora.


Liverpool, Chelsea na Juventus nazo hazipo kwenye nafasi ngumu ya kupenya, lakini mashaka makubwa yapo Atletico Madrid, ambao wanaweza kuaga mapema tu michuano hiyo sawa na ilivyo kwa wakali wa Serie A msimu huu, Napoli.

Real Madrid inayoonekana kuwa kwenye ubora duni msimu huu, watahitaji kushinda ugenini kwa APOEL kujihakikishia nafasi, wakati wenzao kwenye kundi lao, vinara Tottenham Hotspur watakuwa na shughuli huko Ujerumani kuwavaa Borussia Dortmund.

Mechi hizo zote zinapigwa leo Jumanne, sambamba na Napoli watakaokuwa nyumbani kuwakaribisha Shakhtar Donetsk, Monaco watakipiga na RB Leipzig, Sevilla na Liverpool, Spartak Moscow na Maribor, Besiktas na Porto na Manchester City wao watakuwa Etihad kuwakaribisha Feyenoord.

Kesho, Jumatano, michuano hiyo itaendelea kwa Man United wakiwa ugenini kwa FC Basel huku huko Turin kukiwa na bonge la mechi kati ya Juventus na Barcelona.

Bayern Munich wakisafiri kuifuata Andetletch, PSG watakuwa nyumbani kuwakaribisha Celtic na Atletico Madrid watakipiga na AS Roma, huku Sporting CP watakuwa mwenyeji wa Olympiakos, Chelsea wakiwa ugenini kwa Qabarag na CSKA Moscow watakuwa kwao kucheza na Wareno Benfica.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: