BAADHI ya wananchi na wafanyabiashara katika Manispaa ya Bukoba,
wameelezea kushangazwa na uhaba wa sukari na kupanda bei kwa bidhaa hiyo
ambayo kwa sasa inapatikana kwa Sh 2,500 hadi Sh 2,700 licha ya kuwepo
kwa Kiwanda cha Sukari cha Kagera wilayani Missenyi mkoani Kagera.
Wananchi hao wamesema bei hiyo ya sukari ni kinyume cha bei elekezi
ya Serikali ambayo iliagiza kilo moja ya sukari iuzwe kwa Sh 1,800.
Anitha John ni mfanyabiashara katika soko kuu la Bukoba anayeuza
bidhaa mbalimbali ikiwemo sukari ambaye amesema sukari imepanda bei na
ameamua kuacha kuuza kwa sababu kwa wakala kilo 50 zinauzwa Sh 100,000
na kwenye stakabadhi wanaandikiwa 90,000 na wakati wa nyuma kilo hizo 50
walinunua kwa Sh 76,000.
“Jambo la kushangaza si kwamba sukari haipo maana sukari inashushwa
na kupelekwa kwenye maghala ukienda kwenye ghala kununua unaambiwa
hakuna sukari, jambo ambalo ni tatizo kwa wafanyabiashara wadogo kama
mimi, vinginevyo Serikali itoe vibali kwa kila mtu akajinunulie
kiwandani ili biashara isikwame,” alieleza John.
Sebastiani Tweyambe ambaye ni mfanyabiashara mwingine wa bidhaa hiyo,
alisema wiki mbili zilizopita sukari iliuzwa kwa Sh 2,000 wakati Rais
John Magufuli alipotoa bei elekezi ya Sh 1,800, sasa baada ya bei
kushuka inazidi kupanda mpaka sasa imefikia Sh 2,400 hadi 2,500 kutokana
na wanavyonunua mzigo.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: