England imepangwa pamoja na Ubelgiji na Tunisia na Panama huku Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wakipewa timu ngumu.


Katika upangaji wa ratiba hiyo England imepangwa Kundi G watakuwa na kibarua kizito dhidi ya Ubelgiji katika kuwania nafasi ya kuongoza kundi hilo.

Kikosi hicho cha Gareth Southgate kitafunga kampeni yake ya kusaka ubingwa wa kwanza wa dunia tangu 1966 kwa kucheza na wawakilishi wa Afrika, Tunisia Juni 18 kwenye Uwanja wa  Volgograd.

England itacheza mechi ya pili dhidi ya Panama, kwenye Uwanja wa Nizhny Novgorod hapo Juni 24 kabla ya kumaliza na Ubelgiji kwenye Uwanaj wa Kaliningrad hapo Juni 28.

Ronaldo na Ureno wamepangwa Kundi B pamoja na mabingwa wa Dunia 2010, Hispania, Iran na wawakilishi wa Afrika, Morocco.

Wakati Messi ataiongoza Argentina katika Kundi D wakiwa na Croatia, Iceland na miamba ya Afrika, Nigeria.

Makundi Kombe la Dunia 2018

Kundi A: Russia, Uruguay, Misri, Saudi Arabia
Kundi B: Ureno, Hispania, Iran, Morocco
Kundi C: Ufaransa, Peru, Denmark, Australia
Kundi D: Argentina, Croatia, Iceland, Nigeria
Kundi E: Brazil, Uswisi, Costa Rica, Serbia
Kundi F: Ujerumani, Mexico, Sweden
Kundi G: Ubelgiji, England, Tunisia, Panama
Kundu H: Poland, Colombia, Senegal, Japan
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: