Manchester United imekubali kulipa ada ya uhamisho wa pauni 64milioni kwa ajili ya Alvaro Morata.
Morata atawasili England kwa ajili ya vipimo Jumatatu kwa mujibu wa magazeti ya Hispania.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid uhamisho wake kwenda Old Trafford umechochewa na kukwama kwa usajili wa Antoine Griezmann kufuatia Fifa kuifungia Atletico Madrid kusajili.
Uhamisho huo umekuwa rahisi baada ya Man United kuthibisha kuachana na Zlatan Ibrahimovic msimu huu.
Morata alianza maisha yake ya soka la kulipwa akiwa chini ya kocha wa sasa Man United, Jose Mourinho, alipokuwa kifundisha Real Madrid mwezi Desemba 2010 alipocheza dhidi ya Real Zaragoza.
Post A Comment: