KOCHA wa Simba, Jackson Mayanja amesema ushindi wa Yanga na Azam
hauwatishi na kwamba kikosi chake kitapambana mpaka dakika za mwisho.
Yanga na Azam zilimaliza mechi zao za viporo juzi, ambapo mabingwa
watetezi Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mgambo JKT na
Azam ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Majimaji.
Akizungumza kwa njia ya mtandao kutoka Zanzibar ilipo
kambi ya Simba, Mayanja alisema bado timu yake ina nafasi nzuri kwenye
ubingwa kwani soka lolote linaweza kutokea.
Ushindi wa juzi umeifanya Yanga kufikisha pointi 62 kileleni mwa
msimamo wa ligi hiyo, Azam ikiwa nafasi ya pili kwa pointi 58 na Simba
iko nafasi ya tatu na pointi 57, timu zote zimebakiza mechi tano
kumaliza ligi.
“Najua ushindi wa Yanga na Azam katika mechi zake umetuweka kwenye
mazingira magumu kwa sababu wenzetu wameshinda mechi nyingi kutuzidi,
lakini bado hiyo siyo sababu ya sisi kukata tamaa, tutapambana mpaka
dakika ya mwisho,” alisema.
Simba kesho ina kibarua kigumu itakapomenyana na Azam kwenye Uwanja
wa Taifa Dar es Salaam. Mechi hiyo inatarajiwa kuwa ngumu na ya vuta
nikuvute kutokana na kila timu kuhitaji ushindi.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: