Mshambuliaji mwenye hasira, Sadio Mane amembwatukia kocha wake, Jurgen Klopp baada ya kumwingiza dakika ya 89, wakati Liverpool ikicheza na Chelsea.


Mane alikosa uvumilivu baada ya kuwekwa benchi kwa dakika 89 katika mchezo wa sare ya bao 1-1kwenye Uwanja wa Anfield.

Klopp alijaribu kumtuliza mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Senegal, ambaye alishindwa kuficha hasira yake na mashabiki waliofurika uwanjani hapo waliona kila kitu.

Kocha huyo wa Ujerumani, Klopp alisema: "Nilimpigia kelele kwa sababu alikuwa katikati ya uwanja wakati mimi nilitaka acheze kama winga wa kulia."

Klopp alikuwa katikati ya mzozo na mchezaji huyo mara tu baada ya kumalizika kwa mchezo huo na kulazimika kumwelewesha alichokuwa anataka kwake.

Bosi huyo wa Liverpool alianza kuwasumbua na kuwabwatukia waamuzi kwa kuchelewasha kufanya mabadiliko ya kumwingiza Adam Lallana.

Lakini licha ya kumalizana na waamuzi, raia huyo wa Ujerumani aliingia tena katika mzozo na Mane mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo wakipishana kauli.

Mane alikasirishwa na kitendo cha kuingia dakika moja kabla ya mchezo kumalizika, akishindwa kuficha hasira zake kwa kucheza dakika chache katika mchezo huo mkubwa.

Liverpool walianza kupata bao la kuongoza kupitia kwa mshambuliaji wa kimataifa wa Misri, Mohamed Salah dhidi ya timu yake ya zamani, likiwa bao lake la 15 msimu huu akiwa na Liverpool.

Lakini Willian aliisawazishia Chelsea zikiwa zimebaki dakika tano mchezo kumalizika, baada ya kumwinulia mpira kipa Simon Mignolet, dakika chache kabla ya mwamuzi Michael Oliver kumzuia Lallana asiingie uwanjani.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: