Taarifa ni kwamba nyota wa Arsenal Mesut Ozil raia wa Ujerumani anadalili kubwa za kutua Barcelona, Januari mwakani na tayari ada yake imetajwa kuwa ni Pauni 20 milioni.


Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29, atamaliza mkataba wake katika klabu ya Arsenal Juni mwakani na uongozi wa klabu yake una wasiwasi kwamba wanaweza kumtoa bure kwa hiyo uweze kano wa kumuuza kwa kiasi hicho cha pesa ni mkubwa.

Katika siku za karibuni kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alisema kuna dalili kubwa mchezaji huyo akarudi Hispania.

Mchezaji huyo alijiunga na Arsenal akitokea Real Madrid mwaka 2013 na amefunga mabao 24 na kutengeneza mabao 93 katika michezo 171 akiwa na kikosi cha Arsenal.  

Habari ni kwamba Barcelona inataka kuongeza kiwango na wameshaanza kuongea na wakala wa Ozil, Dr ErkutSogut. Lakini imefahamika kuwa kuna klabu nyingine sita ambazo zinamwania mchezaji huyo katika dirisha la usajili la Januari.

Imefahamika kuwa mchezaji huyo atapewa mkataba ambao utamalizika 2020.

 Barcelona kwa sasa ina nguvu katika La Liga ikiwa inashika nafasi ya kwanza kwa tofauti ya pointi nne baada ya kucheza mechi 12. Hata hivyo wanataka kuongeza moto katika kikosi
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: