Kocha Antonio Conte ameingia matatani kwa mara nyingine, baada ya kuibua mzozo na beki kisiki David Luiz.


Conte na Luiz walitoleana maneno makali kwenye mazoezi, Chelsea ilipokuwa ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United.

Libero huyo wa kimataifa wa Brazil, juzi alikuwa jukwaani katika mchezo walioshinda bao 1-0 dhidi ya Man United kwenye Uwanja wa Stamgord Bridge.

Uamuzi wa kumuweka benchi Luiz umeanza kupigiwa kelele na wadau wa soka akiwemo mchambuzi maarufu Gary Neville.

Nahodha huyo wa zamani wa Manchester United, alisema Conte anaweza kufukuzwa kwa uamuzi mbaya wa kumuweka benchi Luiz.

Hii ni mara ya pili kwa kocha huyo kuibua mzozo na mchezaji wake, awali alimtenga Diego Costa kabla ya kumpiga bei Atletico Madrid.

"David ana ushawishi mkubwa ndani ya vyumba vya kuvalia nguo kama John Terry, endapo ataendelea kusugua benchi kwa wiki mbili au tatu huku kamera zikiendelea kumuonyesha jukwaani, Conte anaweza kufukuzwa,"alisema Neville.

Muda mfupi baada ya kuibuka mzozo huo, Conte alidai mchezaji huyo atasota benchi muda mrefu kwa madai ya utovu wa nidhamu.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: