Paris Saint-Germain wamekutana na wakala wa Philippe Coutinho jana jijini London kujadili kuhusu uwezekano wa uhamisho wake mwisho wa msimu kwa mujibu wa taarifa za Ufaransa.


Matajiri hao wa Paris wameweka wazi lengo lao la kwanza ni kuipata saini ya Mbrazil huyo wakati wakiendelea kutumia fedha kujenga kikosi chao.

Gazeti la Telefoot limedai kuwa wakala Kia Joorabchian amekutana na mkurungezi wa ufundi wa PSG, Antero Henrique kujadili kuhusu Coutinho na wachezaji wengine wawili.

Taarifa hiyo imewataja nyota wa Inter Milan, Joao Mario na kiungo Mbrazil Wendel kuwa sehemu ya uhamisho wao.

PSG imevunja rekodi ya usajili wa pauni198milioni kumnunua Neymar msimu uliopita, lakini bado hawajaonyesha kwamba wanania ya kuacha kutumia fedha.

Taarifa hiyo itaamsha hisia kwa Barcelona ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakihusishwa na kutaka kumnunua Coutinho.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: