AFYA ya faru mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani anayehifadhiwa katika Bonde la Ngorongoro, maarufu kwa jina la Fausta, imeimarika baada ya kuugua kwa muda mrefu katika eneo maalumu alikohifadhiwa.


Faru Fausta amekuwa kivutio kikubwa kutokana na umri wake.

Kwa sasa faru huyo ametengwa kwa ajili ya kutibiwa majeraha makubwa aliyokuwa nayo kutokana na changamoto za porini.

Kwa mujibu wa daktari anayemuangalia faru huyo, Dk. Francis Makali, Fausta ana umri wa miaka 52.

β€œFausta alikuwa na majeraha makubwa ambayo yalihatarisha maisha yake," alisema Dk. Makali, lakini "hivi sasa afya yake imeimarika na anaendelea vizuri.”

Alisema licha ya afya ya faru huyo kuimarika, hakuna mpango wa kumuachia arudi nyikani kutokana na umri wake kuwa mkubwa pamoja na uoni hafifu wa jicho moja.

Hivi karibuni faru fausta alizua gumzo bungeni,baada ya taarifa kusema kuwa matibabu yake na malisho yake kwa siku ni zaidi ya milioni 50
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: