Baada ya Neymar na Messi kupokea vitisho kundi la ISIS limemtumia ujumbe huo mwanasoka bora wa mwaka wa Fifa, Cristiano Ronaldo


Kundi la dola la Kislamu limeendelea kutuma ujumbe wa vitisho kwa nyota wanasoka baada ya kumtumia ujumbe huo Ronaldo katika kuelekea katika fainali za Kombe la Dunia 2018, Russia.

Neymar, Lionel Messi na kocha wa Ufaransa, Didier Deschamps tayari wameshapokea ujumbe wa vitisho kutoka kwa ISIS kupitia picha zilizochapishwa kwenye tovuti yao.

Katika tovuti SITE Intel Group imeonyesha picha ya Ronaldo akiwa amepiga magoti huku jicho lake moja likiwa jeusi na nyuma yake amesimama mtu mwenye kisu mkononi.

Picha hiyo ya Ronaldo chini yake iliwekwa ujumbe uliosomeka "Neno letu ni hiki unachokiona, siyo kile unachosikia," ulisomeka ujumbe huo na kuongeza. "Kwa hiyo, subiri, tunakusubiri.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: