Kiungo wa Singida United, Deus Kaseke, amekiri mchezo ujao dhidi ya Yanga utakuwa wa aina yake kutokana na kuzikutanisha timu zenye wachezaji bora.


Singida United itaikaribisha Yanga Jumamosi katika mchezo utakofanyika Uwanja wa Namfua, Singida ambao utatumika kwa mara ya kwanza baada ya kufanyiwa ukarabati.

 Kaseke, ambaye msimu uliopita aliitumikia Yanga, alisema atakuwa na kibarua kigumu kukutana na timu yake ya zamani katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Alisema mkakati wa Singida United ni kupanda katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi, hivyo lazima wapambane kuhakikisha wanashinda mchezo huo baada ya kutoka suluhu juzi na Mtibwa Sugar ugenini.

"Nawaheshimu Yanga ni timu nzuri ina wachezaji wenye ubora kama Singida United, itakuwa mechi bora," alisema mshambuliaji huyo wa pembeni.

Kaseke alisema kutoka suluhu na Mtibwa Sugar walirejea nyumbani Singida kujipanga kwa mchezo huo aliodai ni muhimu kupata pointi tatu.

Mchezo huo utakuwa wa pili kwa timu hizo kupepetana mwaka huu na katika mechi ya kirafiki Singida United ililala mabao 3-2.

Mchezo huo unatarajia kuwa na mvuto wa aina yake kwa kuwa Singida ina wachezaji kadhaa waliowahi kuwika Yanga kipa Ali Mustapha 'Barthez', Nizar Khalfan, Kigi Makassi, Atipele Green na Kaseke.

Singida United inanolewa na kocha wa zamani wa Yanga Mdachi Hans Van Der Pluim, aliyekuwa kipenzi cha mashabiki wa klabu hiyo ya Jangwani.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: