BEKI wa zamani wa timu ya Taifa ya Rwanda (Amavubi) na klabu ya APOP Kinyras Peyias ya Cyprus, Ndikumana Hamad "Katauti" (39), amezikwa jana katika mji wa Nyamirambo, Rwanda imeelezwa.


Katauti ambaye hadi anafariki alikuwa Kocha Msaidizi wa timu ya Rayon Sports inayoshiriki Ligi Kuu Rwanda, alifariki dunia usiku wa kuamukia jana akiwa nyumbani kwake Kigali.

Beki huyo ambaye aliwahi kuwa mume wa msanii wa filamu nchini, Irene Uwoya, imeelezwa kuwa juzi jioni alishiriki katika programu ya mazoezi ya timu yake na wala hakuonekana mgonjwa.

"Bado mpaka sasa hatujajua nini chanzo cha kifo chake, lakini anatarajiwa kuzikwa leo (jana)," alisema kwa kifupi Bonnie Mugabe, ambaye ni Afisa Habari wa Chama cha Soka cha Rwanda (FERWAFA).

Mbali na klabu mbalimbali za ulaya alizowahi kuitumikia beki hiyo, pia aliwahi kuichezea timu ya Stand United ya Shinyanga, Tanzania.

Beki huyo alikuja nchini mara ya mwisho na kikosi cha Rayon Sports kucheza na Simba katika mechi ya kirafiki ya Simba Day iliyofanyika Agosti 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na wageni hao kufungwa 1-0.

Katauti ambaye alianza kuitumikia Amavubi tangu mwaka 1998, alikuwa kwenye kikosi kilichoisaidia timu hiyo kufuzu kwa mara ya kwanza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zilizofanyika mwaka 2004.

"Tumepoteza watu wawili muhimu, pumzika kwa amani Katauti na Gangi ( nyota mwingine wa Amavubi-Hategekimana Bonaventure)," alisema Haruna Niyonzima, kiungo wa Simba.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: