Serikali imesema kuwa tozo iliyowekwa kwenye Daraja la Kigamboni itaendela kuwepo kwa kuwa imefuata utaratibu wa kisheria na kanuni.


Kauli hiyo imetolewa jana  Novemba 15, 2017 Bungeni mjini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Sera, Bunge, Ajira, Kazi, Vijana na Ulemavu, Jenista Mhagama baada ya Mbunge Zainabu Ndolwa kuhoji jambo hilo,

"Je ni lini serikali itasitisha tozo za daraja la Kigamboni ili liweze kutumika kama madaraja mengine Ruvu na Wami?

β€œDaraja la kigamboni limejengwa na mfuko wa jamii wa NSSF ni kivuko ambacho kinachofanya kazi kama vivuko vingine tulivyo navyo nchini na vivuko vingine pia vimeweka mfumo wa utozaji wa Tozo kidogo ili kuhakikisha kwamba vivuko vile vinaendela kulindwa na kukarabatiwa ili kuendelea kufanya kazi kwahiyo nisema kwamba Tozo iliyowekwa katika Daraja la Kigamboni imefuata utaratibu wa Kisheria na Kikanuni na hivyo itaendelea kuwepo,” amesema Jenista.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: