KAMA ulikuwa unaichukulia poa Yanga pole yako, ni  kwa sababu pale Jangwani kwa sasa kumenoga kinoma.


Yanga inayohaha kuukarabati Uwanja wa Kaunda ili kuondokana na kujitia hasara ya kujitakia, kwa sasa ipo katika mstari na Katibu Mkuu wake Boniface Mkwasa amekiri bado kidogo tizi litaanza kupigwa Jangwani.

Mkwasa alisema makundi 68 ya Yanga ya mitandao ya kijamii ya Facebook na Whatsapp, yamechangia kiasi cha fedha za kutosha mpaka sasa kwa ajili ya maandalizi ya ukarabati wa uwanja wao.

β€œNiweke wazi kwamba tumefikia sehemu nzuri, wanachama wanajitolea kwa hali na mali, ndani ya siku tatu watajua kiasi kilichopatikana na bado tunawaomba waendelee kujitolea ili klabu yao iendelee kuwa mfano nchini kuanzia uwanjani mpaka umiliki wa vitu vyetu,” alisema Mkwasa.

Aliongeza amekutana na viongozi wanaosimamia eneo la Mto Msimbazi, waliosaidia kutanua mtaro ili kupunguza mafuriko na  walimuunganisha wa watu wa Tanroads waliowapa kifusi cha kusaidia ukarabati wa uwanja huo.

β€œTanroads wametupa kifusi, tunatafuta namna ya kukifikisha hapa, tayari vifusi vingine vimeishafika na tumesaidiwa namna ya kutanua mtaro wa kupunguza mafuriko kandokando ya uwanja wetu,” alisema Mkwasa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: