ads

Ratiba ya Kombe la Shirikisho Afrika imetoka na Simba imepata bahati yah kupangwa na timu laini au kibonde kutoka Djibouti.


Simba imepangwa kuanza Gendamarie, timu ambayo imekuwa ni moja ya vibonde katika michuano ya Kagame ambayo ni maalum kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Pamoja na kuanza na kibonde, Simba itatakiwa kujipanga kwelikweli kama itafanikiwa kusonga mbele katika hatua hiyo.

Hatua inayofuata inaonyesha itakuwa ngumu kwa kuwa Simba ikisonga mbele itakutana na timu ya Zambia au Misri.

El Masry ya Misri itakutana na Green Buffaloes ya Zambia na mshindi wa hapo atakutana na mshindi kati ya Simba dhidi ya Gendamarie.

Ligi ya Mabingwa Afrika

Unaweza kusema ratiba ya mwanzo ya Ligi ya Mabingwa Afrika si ngumu kwa Yanga.

Shirikisho la Soka Afrika (Caf), limeipangia Yanga kuanza na St Louis ya Shelisheli, timu ambayo hauwezi kusema ni mlima mrefu kwa kwa Yanga.


Ingawa Yanga watapaswa kuwa makini kwa kuwa ni soka na soka la Shelisheli limekuwa likipanda, lakini haiwezi kuwa kazi itakayowashinda wakiamua “lazima” wasonge mbele.

Iwapo Yanga itasonga mbele katika hatua hiyo baada ya kufanya vizuri katika mechi mbili dhidi ya St Loius, inatarajia kukutana na mshindi kati ya El Merreikh ya Sudan au Township Rollers ya Botswana.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: