Umoja wa Vijana wa chama cha Zanu PF nchini Zimbabwe umeomba Rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe aruhusiwe kuongoza nchi hiyo hadi atakapokutwa na umauti.


Mapendekezo hayo yamekuja wakati huu ambapo wanachama wengi katika chama hicho tawala kwenye majimbo nchi nzima walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita na kuamua kuitisha mkutano wa dharura mwezi Desemba kuzungumzia sakata la Mugabe kushindwa kumuandaa mrithi wake kwa miaka 37 aliyokaa madarakani.

Kwa mujibu wa gazeti la NEWS24 taarifa zimeeleza kuwa vijana hao wamefikia maamuzi hayo ya kuwasilisha maombi hayo baada ya taarifa kutoka kwenye kamati ya nidhamu ya Chama hicho kuwasilisha jina moja la mrithi wake ambapo ametajwa kuwa ni mke wa Rais Mugabe, Grace Mugabe.

Hata hivyo, tayari mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Zanu PF, Mubuso Chinguno amesema chama hakina mgombea mwingine zaidi ya mzee Mugabe (93) licha ya kuwa umri wake umemtupa mkono.

β€œMugabe ni Rais wetu wa maisha, hatuna tatizo nae hata akifia ofisini kwa hiyo tunakaribisha mapendekezo haya mapya ya kuwepo kwa kongamano kujadili hilo na baadae kuwasilisha kwenye mkutano mkubwa wa mwaka mwezi Desemba mwaka huu.” amesema Mubuso Chinguno kwenye mahojiano yake na gazeti la NEWS24.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: