Miongoni mwa madiwani waliojiuzulu wakiwa Chadema kwa kile walichosema ni kumuunga mkono Rais John Magufuli, wameanguka kwenye kura ya maoni ya CCM ngazi ya kata.


Kuanguka kwa madiwani hao ni kinyume cha ahadi ya Rais Magufuli aliyoitoa akiwa mkoani Arusha ambako alipendekeza madiwani hao wapewe kipaumbele ndani ya CCM.

Rais Magufuli pia alipendekeza madiwani hao wapewe kipaumbele cha kupitishwa kugombea udiwani kupitia CCM katika uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika Novemba 26 ukihusisha kata 43 nchini.

Katibu wa Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Shaaban Mdoe amesema kuanguka kwa madiwani si hoja kwa sababu hiyo ni ngazi ya kata na bado mchakato wa uchaguzi unaendelea.

Mdoe amesema baada ya kura ya maoni ndani ya kata, majina yatapelekwa katika Sekretarieti ya Wilaya kwa ajili ya mchujo na baadaye ngazi ya mkoa ili kupendekeza jina la mgombea, kazi itakayokamilika kabla ya Oktoba 20 mwaka huu.

Walioangushwa katika kura ya maoni ni Anderson Sikawa aliyekuwa diwani wa Leguruki, Greyson Isangya (Maroroni),  Josephine Mshiu (Viti Maalumu), Emmanuel Mollel (Makiba) na Japhet Jackson (Embuleni).

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: