Robert Mugabe alijiuzulu Novemba 21 baada ya kuahidiwa kinga ya kutoshtakiwa, kulipwa dola za Marekani 10 milioni kwa mkupuo, mshahara wa kila mwezi, matibabu, usalama wake pamoja na ulinzi wa mali zake, gazeti la Independent limeandika.


Uchunguzi uliofanywa na Independent umefichua kwamba watu wa Mugabe walioshiriki katika mazungumzo yaliyowezesha yeye kuondoka walifanikiwa kufikia makubaliano na majenerali kuhakikisha mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 93 haendi kuishi uhamishoni bali afurahie kustaafu kwake nchini Zimbabwe na apate marupurupu yake.

“Serikali itamlipa Mugabe dola 5 milioni kwa mkupuo na kisha kiasi kinachosalia atakuwa akilipwa kwa mafungu,” chanzo kimoja kimesema. “Mugabe atapatiwa matibabu pamoja na mshahara kamili kila mwezi. Na ikiwa atafariki mkewe atakuwa analipwa nusu mshahara kila mwezi.”

Mugabe alifanya majadiliano ili aweze kuondoka salama kupitia timu ya wapatanishi ambayo ilijumuisha kasisi wa Kikatoliki, Fidelis Mukonori na gavana wa zamani wa RBZ Gideon Gono. Mukonori alisema katika mahojiano kwamba wajibu wake ulikuwa kuwa mpatanishi kati ya majenerali na Mugabe.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: