Baada ya kufutwa kazi aliyekuwa kocha wa Bayern Munich Carlo Ancelotti ameishukuru bodi ya timu hiyo kwa kumwamini pamoja na ushirikiano waliompa katika kipindi chote alichofundisha timu hiyo.


Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ancelotti ameandika β€œImekuwa heshima kubwa kuwa sehemu ya historia ya Bayern Munich. Napenda kuishukuru Klabu, Wachezaji na zaidi mashabiki wa kushangaza ambao sijawahi kukutana nao tangu nianze kufundisha soka”.

Mtalaam huyo wa ufundi mwenye miaka 58 alipoteza kibarua chake juzi  mchana baada ya bodi ya Bayern Munich kuketi na kocha huyo na kuazimia kutoendelea na mkataba wake uliokuwa unamalizika 2019.

Baadhi ya wachezaji wa Bayern Munich Thiago Alcantala, Frank Ribery, Robert Lewandowski na Arturo Vidal wamemshukuru Ancelotti kila mmoja akieleza kwa namna ambavyo amefaidika kuwa chini ya kocha huyo kwa msimu mmoja
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: