WAKATI wanatarajia kutua Shinyanga leo kwa ajili ya mechi dhidi ya wenyeji wao Stand United itakayofanyika keshokutwa, Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, amesema kuwa hakuna kocha wa soka ambaye yuko "mahali salama" duniani.


Akizungumza  jana, Omog, alisema kuwa matokeo ya mpira huwa hayafurahishi kwa asilimia 100 na hiyo huepeleka makocha kufukuzwa na kuajiriwa kila mara katika klabu mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Omog alisema anafahamu kuna mazungumzo mbalimbali yanayoendelea kuhusiana na ajira yake, lakini akaweka wazi kuwa hakuna uamuzi wowote ambao utafanywa utamshtua.

"Hakuna kocha ambaye yuko mahali salama, ndiyo sababu kila siku timu zinafanya mazoezi, ili kurekebisha makosa yanayojitokeza, na pia kuongeza uwezo wa wachezaji, ninamatumaini mambo mazuri yanaweza kukuondoa au kukubakisha kwenye klabu," alisema Omog.

Mcameroon huyo aliongeza kuwa mechi zote za Ligi Kuu Tanzania Bara zina ushindani kwa sababu wachezaji wameanza kuelewa na kuthamini umuhimu wa kazi wanayoifanya kutokana na kujifunza yale yanayotokea kwa wachezaji wa klabu za Ulaya.

"Changamoto na michakato tunayoishuhudia katika soka la Ulaya, inasaidia kusukuma maendeleo kwenye klabu zote nchini, ingawa hatuwafikii, lakini tunavyojifunza vinatusaidia," Omog aliongeza.

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Simba yenye pointi nane iko katika nafasi ya nne ikitanguliwa na vinara Mtibwa Sugar wenye pointi 10 sawa na mabingwa wa Kombe la Kagame, Azam FC na Singida United ambao wana pointi tisa, yenyewe ni ya nne.

Baada ya mechi zitakazochezwa Jumapili, ligi hiyo itasimama kwa muda, ili kupisha maandalizi ya timu ya Taifa (Taifa Stars) ambayo itaikaribisha Malawi ifikapo Oktoba 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: