Mtayarishaji wa muziki anayesumbua masikio ya wapenda burudani kwa mdundo wa ngoma mpya ya Alikiba 'Seduce Me', Man Water amedai wakati huu ambao amerudi kwa kasi na ngoma kubwa ndiyo muda ambao atamrudisha msanii 20 Percent.


Akiwa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio kwenye 'media tour' ya Alikiba , Man water amesema mwaka huu anaamini ndiyo wakati wa studio yake ya Combination Sound kurudi hewani kama zamani na kudai ndiyo wakati wake baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.

"Combination kuna mambo makubwa tuliyoyaandaa, ikiwepo kazi hizi za Kiba ambazo zimeanza kutoka lakini mashabiki zetu tunawaahidi makubwa. 20 Percent lazima arudi mapema iwezekanavyo kwenye hili hili vugu vugu la Alikiba hapa ndiyo na yeye atapita na nawaahidi lazima afanye vizuri,"  alisema Man Water 

Man Water pamoja 20 Percent walimaliza ugomvi wao mnamo Oktoba 05, 2013 baada ya kudumu kwenye mgogoro na msanii huyo kwa muda usiopungua mwaka mmoja kwa kile alichokiita kupishana lugha wakati wa kufanya kazi pamoja ambapo mwaka jana alipotaka kumrejesha kwenye 'game' mapokezi hayakuwa mazuri hivyo kumfanya akae benchi kwanza.


ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: