
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Msanii wa muziki wa bongo fleva Alikiba ambaye amepewa cheo cha 'Mfalme' na mashabiki wake, amedhihirisha kuwa mashabiki hawakukosea kumpa cheo hicho, kwa kuvunja rekodi ya kutazamwa kwa video yake kwa mara nyingi zaidi ndani ya muda mfupi.
Kwenye ukurasa wake wa instagram, Alikiba ambaye siku ya Ijumaa ameachia video ya wimbo mpya ya 'Seduce me', ameweka post akiwashukuru mashabiki wake kwa kufanikisha kuvunja rekodi hiyo.
"Ahsanteni sana kwa upendo, nisingebarikiwa zaidi na kupendelewa bila nyinyi, nyinyi ni wa maana sana kwangu na nafanya haya kwa ajili yenu", aliandika Alikiba.
Pamoja na hayo kwenye ukurasa wa instagram wa kampuni kubwa inayosimamia muziki wa Alikiba ya Rockstar. imeandika kuhusu rekodi ya video hiyo ambayo bado inaendelea kushika namba moja kweny video zinazotrend.
Historia ya kuvunjwa rekodi imewekwa, Mfalme Kiba na wimbo wake mpya wa 'Seduce me' umekuwa wa kwanza na kipee kwa msanii wa Afrika Mashariki kufikia kutazamwa mara milioni 1 kwenye Vevo/YouTube ndani ya masaa 38 tu, ina 'trend'namba 1 Tanzania na namba 1 Kenya kwa 'weekend' nzima, rekodi imevunjwaβ, iliandika Rockstar.
Post A Comment: