
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Bodi ya Ligi (TPLB) ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefanya mabadiliko ya ratiba ya michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara kwa baadhi ya mechi ili ziweze kupisha mchezo wa kirafiki baina ya Taifa Stars dhidi ya Botswana.
Mechi ambazo zimefanyiwa mabadiliko ni kati ya Tanzania Prisons na Majimaji ya Songea; Azam FC na Simba, Njombe Mji na Young Africans; Mtibwa Sugar na Mwadui FC, Lipuli na Stand United; Singida United na Mbao; Kagera Sugar na Ruvu Shooting wakati Mbeya City na Ndanda FC ambazo sasa zitachezwa Septemba 6, 2017.
Michezo mingine ambayo imesogezwa hadi Septemba 11, 2017 ni kati ya Azam na Kagera Sugar wakati Mbao na Tanzania Prisons utachezwa Septemba 21, mwaka huu.
Kadhalika mechi nyingine zitachezwa Oktoba 11, mwaka huu ni kati ya Mbao na Azam FC; Kagera Sugar na Mwadui; Mbeya City na Ruvu Shooting; Ndanda na Singida United.
Tarehe hiyo pia Oktoba 11, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya Njombe Mji na Simba; Mtibwa na Tanzania Prisons; Lipuli na Majimaji wakati Stand United na Young Africans watacheza Oktoba 12, mwaka huu.
Novemba 15, 2017 Mbao itacheza na Young Africans; Kagera na Mbeya City; Stand United na Azam; Mwadui na Ruvu Shooting; Singida na Njombe Mji; Lipuli na Tanzania Prisons; Mtibwa Sugar na Majimaji wakati Novemba 16, Ndanda itacheza na Simba.
Kwa upande mwingine, Taifa Stars inatarajiwa kushuka dimbani mwishoni mwa juma hili kuvaana na timu ya Botswana katika mechi ya kirafiki itakayopigwa katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Post A Comment: