Rais John Magufuli amewataka viongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)  kutokuwa na kigugumizi cha kuchukua hatua pale wanapokuwa na ushahidi dhidi ya watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.


Ametoa agizo hilo jana Agosti 28, alipotembelea na kuzungumza na wafanyakazi wa Takukuru katika ofisi za makao makuu ya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

β€œKuna mambo mengi ya hovyo yanafanyika, tumehakiki pembejeo za ruzuku na kubaini madai ya Sh48 bilioni ni hewa, tumebaini wafanyakazi hewa zaidi ya 19,500, tumebaini kaya masikini hewa 56,000 zilizopaswa kupata fedha Tasaf, tumebaini wanafunzi hewa 5,850 waliotakiwa kupata mkopo, kuna vichwa vya treni 11 vimeletwa bila kuwepo mkataba na mengine mengi, haya yote yanafanyika kwa rushwa, nataka kuwaona mnachukua hatua stahiki,”amesema.

Taarifa ya Ikulu imesema Rais ameeleza kuwa na imani na Takukuru na amewataka wafanyakazi wake kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, uzalendo na uadilifu, akiahidi Serikali kufanyia kazi changamoto zinazowakabili.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: