Msanii wa filamu maarufu duniani na raia wa Marekani, Cynthia Rothrock, maarufu Lady Dragon, ametua kutalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.


Cynthia aliyewahi kushinda tuzo tano za filamu duniani kupitia filamu zake za mapigano, amefikia katika hoteli ya Grumeti Serengeti inayomilikiwa na  bilionea wa Marekani, Paul Tudor.

Msanii huyo ambaye ameigiza zaidi ya filamu 31, miongoni wa zilizompa umaarufu ni Lady Dragon Xtreme Fighter na Deadliest Art.

Tangu atue nchini juzi Agosti 26, picha zake zimesambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii duniani.

Hata hivyo, kama ilivyokuwa kwa mchezaji maarufu wa Uingereza, David Backham, safari ya Cynthia ni ya mapumziko binafsi.

Akizungumzia ujio wa msanii huyo mwenye mkanda mweusi katika mchezo wa karate, Meneja Uhusiano wa Tanapa, Pascal Shelutete, amesema umetokana na kazi kubwa ya Serikali, Tanapa na wadau wengine kuitangaza Serengeti.

Shelutete amesema wasanii wengine wengi wakubwa duniani wanatarajiwa kuingia nchini, kutalii kama ambavyo imetokea mwaka huu.

β€œMwaka huu umekuwa mzuri katika utalii nchini, tumepata watalii wengi maarufu duniani, wakiwemo wachezaji mpira, wasanii wa filamu na viongozi wa kisiasa,” amesema.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: