ads

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amefunguka na kusema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaongeza mishahara ya wafanyakazi mwezi huu Novemba kama Rais Magufuli alivyoagiza


Dkt. Abbasi amesema hayo wakati akitoa tathmini ya miaka miwili ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli toka alipoapishwa Novemba 5, 2015 na kusema kuanzia mwezi huu wafanyakazi wataongezewa mishahara yao. 

"Mwezi huu mishahara ya wafanyakazi wa Serikali itaongezwa kama Rais Magufuli alivyoahidi" Dkt. Hassan Abbasi

Mbali na hilo Msemaji wa Serikali amesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais Magufuli wameweza kufanikisha kufufua viwanda 17 kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina pia amedai ndani ya muda huo Serikali imeanzisha Mahakama ya Mafisadi ambapo mpaka sasa kesi 3 za uhujumu uchumi zimeanza kusikilizwa.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: