ads

Rais John Magufuli amemwandikia barua waziri mkuu wa Canada kuulizia kuhusu ndege ya Bombadier, inayoshikiliwa nchini humo na kumtaka ashughulike suala hilo kwa haraka.


Akizungumza katika uzinduzi wa Uwanja wa ndege mjini Bukoba leo Jumatatu Novemba 6, Rais Magufuli amesema amemtuma pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju kwenda Canada kushughulikia suala hilo kisheria.

"Nimemwandikia barua waziri wa Canada kuulizia kwanini ndege yetu inakaa zaidi ya miezi sita, tumechoka kusubiri. Nimemtuma pia mwanasheria mkuu ili akapambane nao kisheria," amesema.

Amesisitiza kwamba kama wameamua kupambana kisheria watapambana na amewataka wanasheria wa Tanzania kushikamana ili kuhakikisha kwamba ndege hiyo inakuja Tanzania.

Rais Magufuli amewaonya wananchi pia kuacha kuzungumza kwenye mitandao ya kijamii. Alisema “ninawaomba watu wa vyama vyote waunge mkono juhudi hizi zinazofanywa na serikali.”

Magufuli ambaye ametimiza miaka miwili tangu achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania amesema ndege zote sita zilizonunuliwa na Serikali zitakuja.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: