Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka watanzania kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho nchi inajitahidi kujikwamua kiuchumi. 


Rais magufuli ameyasema hayo alipokuwa akihutubia kwenye sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, zilizofanyika katika uwanja wa Amani Zanzibar.

Kwenye hotuba hiyo Rais Magufuli amesema nchi yoyote inyopitia mabadiliko ya kiuchumi, ni kawaida kupitia kwenye wakati mgumu hivyo watanzania ni vyema wakawa na uvumilivu na subira, ili kuingoja neema itakayokuja.

"Licha ya ukweli kutokana na hatua tunazozichukua za kuwabana mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma, wapo wananchi wa kawaida ambao si wezi wala mafisadi wanaoathirika, hili ninalifahamu, lakini kama kweli tunataka kupambana na wizi na ubadhirifu pamoja na kuleta maendeleo kwa nchi yetu, athari hizi hatuwezi kuzikwepa, mabadiliko ya aina yoyote ile lazima yana athari kama hizi, lakini jambo la kututia moyo ni kwamba athari hizi mara nyingi ni za kipinzdi kifupi", amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameendelea kwa kusema kwamba ..."Mabadiliko ni magumu mwanzoni, yatakuwa machungu yanapofikia katikati, lakini mwishoni matokeo yake ni mazuri au ni matamu, hivyo nawaomba wananchi na watanzania tuvumile katika kipindi hichi cha mpito, baada ya muda mfupi mambo yatakuwa mazuri, lakini hata kama hayatakuwa mazuri hivi karibuni, watoto na wajukuu zetu watanufaika, na huo ndio uzalendo".

Pamoja na hayo Rais Magufuli amesitiza kwamba uchumi wa nchi unaendelea kukua, na kwamba wanaosema hivyo ni waongo na wazushi, na kuwataka watanzania wawapuuze.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: