
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
WAMETEPETA! Hatimaye yale mazungumzo mazito na marefu baina ya serikali na kampuni ya Barrick Gold kuhusiana na shughuli za uchimbaji wa dhahabu nchini, yamefikia mwisho huku kila upande ukiridhia mambo kadhaa yakiwamo takribani 18 yenye kuashiria ushindi kwa taifa.
Kuanzishwa mfuko wa kutafiti mchakato wa kujengwa nchini kwa kiwanda cha kuchakata mchanga wa dhahabu (makinikia), kuwapo kwa mgawanyo sawa wa asilimia 50 kila upande wa faida itokanayo na shughuli za migodi ya Barrick na umiliki wa serikali wa hisa asilimia 16 katika migodi ya kampuni hiyo kama inavyotaka sheria mpya ya madini na rasilimali za nchi ya mwaka 2017, ni miongoni mwa mambo hayo takribani 18 yaliyoridhiwa na pande zote mbili.
Katika mazungumzo hayo yaliyodumu tangu Julai 31, mwaka huu, serikali ilikuwa ikiwakilishwa na wataalamu wanane wakiongozwa na Waziri wa Sheria na Katiba, Prof. Palamagamba Kabudi, huku Barrick wakiwa na timu iliyoongezeka idadi ya wajumbe wake kutoka vigogo 14 waliokuwapo awali wakiongozwa na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni hiyo, Prof. John Thornton, hadi kufikia 25.
Maridhiano baina ya wajumbe wa pande hizo mbili, yalifikiwa kwa pamoja na timu za maprofesa Kabudi na Thornton mbele ya Rais John Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Uchambuzi wa Nipashe ulionyesha kuwa karibu mambo yote aliyokuwa akiyapigania Rais Magufuli kabla hata ya kuwa Rais yaliridhiwa na vigogo wa Barrick walioshiriki mazungumzo hayo.
Kabla ya kuingia madarakani Novemba 5, 2015, Rais Magufuli alikaririwa mara kadhaa, hasa kwenye mitandao ya kijamii, akipania kukomesha upotevu mkubwa wa mapato kwa taifa kupitia rasilimali ya madini, hasa juu ya usafirishaji wa makinikia kwenda nje ya nchi badala ya kazi hiyo ya uchenjuaji kufanyika nchini.
Awali, wakati akiwasilisha muhtasari wa maridhiano hayo, mwenyekiti wa kamati iliyoongoza mazungumzo ya pande mbili, yaliyodumu takribani miezi mitatu, Prof. Kabudi, alieleza namna majadiliano yalivyokuwa magumu na marefu, lakini akimshukuru Rais Magufuli kwa kumpa moyo yeye na wenzake wakati wote katika kuhakikisha kuwa maslahi ya taifa yanazingatiwa.
“Kuna wakati nilitetereka sana katika kazi hii ila nakushukuru Mheshimiwa Rais ulinitia moyo. Kazi hii ilihatarisha hata uhusiano wetu hivyo ili kuimarisha uhusiano wa sasa na baadaye ilibidi kusimama imara,” alisema Prof. Kabudi na kuongeza:
“Tunakushukuru sana Mheshimiwa Rais Magufuli … wenzetu walitoka kampuni kubwa, na benki kubwa, sisi ni timu ya watu wanane tu.”
Pia alisema: “Usingetupa imani hiyo, ungeingia katika mtego wa kuleta wataalamu kutoka nje ili watusaidie… Mheshimiwa Rais nakushukuru sana, tena sana, kwa kutupa imani yako…Mungu akubariki.”
Akizungumza baada ya kutia saini makubaliano hayo, Prof. Thornton alimsifu Rais Magufuli na serikali yake kwa namna walivyoshughulikia suala hilo hadi kufikia maridhiano.
Aidha, Prof. Thornton alimpongeza pia Rais Magufuli kwa msimamo wake unaojenga misingi ya biashara ya kuaminiana na uwazi, ambayo ni muhimu na ya namna yake kwa biashara katika karne hii ya 21.
Prof. Thornton alisema Barrick Gold watazingatia makubaliano hayo na wanaamini kuwa yamefungua ukurasa muhimu utakaowezesha kufanya biashara kisasa.
Baada ya kushuhudia maridhiano hayo Rais Magufuli aliwapongeza wajumbe wa timu zote mbili za mazungumzo kwa kazi kubwa waliyoifanya na kufikia makubaliano hayo, huku pia akimpa pongezi ya kipekee Prof. Thornton kwa nia yake thabiti ya kukubali kufanyika kwa mazungumzo na kukubali mambo yaliyofikiwa.
Rais Magufuli alisema makubaliano hayo yataisaidia nchi kuzalisha ajira zaidi, kupata manufaa mbalimbali yanayostahili ikiwamo fedha za kugharamia huduma za kijamii kwa wananchi na pia yanajenga msingi imara ambao utaiwezesha Tanzania kunufaika na rasilimali zake za madini.
Aidha, Rais Magufuli aliwataka Watanzania wawe mstari wa mbele katika kuiunga mkono serikali kupigania rasilimali zilizopo ili mwishowe zinufaishe taifa.
“Hakuna mtu atakayekuja kututengenezea Tanzania yetu. Tuna wajibu wa kufanya mabadiliko ya kweli, hakuna malaika wataokuja kutuletea mabadiliko, mngeweza kukaa kimya, kuhongwa, lakini mlisimama kwa manufaa ya taifa, hatuwezi kuendelea kuwa shamba la bibi, lazima tusimamie rasilimali zetu,” alisema.
Rais Magufuli alisitiza kuwa Tanzania ni tajiri, hivyo kila Mtanzania atimize wajibu wake katika kufanikisha mabadiliko ya kuelekea kufanikiwa kiuchumi kupitia rasilimali nyingi zilizopo.
“Nchi yetu ni tajiri…kila Mtanzania mahali alipo ni lazima ajue ana wajibu wa kufanya mabadiliko,” alisema na kuongeza:
“Sasa kwa mara ya kwanza tangu dunia iundwe, sisi tutachukua faida hamsini kwa hamsini.
Tutapeleka kwenye madawa, huduma za kijamii na kadhalika…lakini pia ile asilimia yetu 16 iko hapo hapo…kodi zitaendelea kulipwa.”
Aidha, Rais Magufuli alisema makubaliano yaliyofikiwa yanapaswa kuwa mfano pia kwa migodi mingine ya dhahabu na madini mengine kama almasi na tanzanite, lengo likiwa ni kuona kuwa wawekezaji wote wanaingia katika mazungumzo na serikali ili kufikia maridhiano kama hayo.
Alionya kuwa mwekezaji yeyote asiyetaka kuzingatia jambo hilo lenye dhamira ya kulinufaisha taifa na rasilimali zake, ni bora aondoke.
“Lakini nataka Profesa (Kabudi)…sasa muanze negotiations (majadiliano) kwenye almasi, kwenye tanzanite… muwaite hao wa tanzanite waje tuzungumze nao. Atakayekataa aondoke, watuachie madini yetu. Tutafanya hivyo hivyo kwenye madini mengine,” alisema Rais Magufuli kabla ya kumwagiza Prof. Kabudi kusimamia suala hilo na kusisitiza kuwa asiyetaka aondoke.
USHINDI MAENEO 18
Mbali na mgawo wa faida wa asilimia 50 kwa 50, hisa za asilimia 16 na kuwapo mfuko kwa ajili ya utafiti wa mchakato wa kujenga kiwanda cha uchenjuaji makinikia, maeneo mengine yaliyoonekana kulinufaisha taifa ni pamoja na la nne ambalo ni Barrick kuweka fedha zao nchini kwa kufungua akaunti kwenye benki zilizopo.
Jambo la tano lililoashiria ushindi kwa taifa kampuni za kutoa huduma kwenye migodi hiyo ziwe za Kitanzania; jambo la sita ni ofisi kuu ya uhasibu ya kampuni ya Acacia (inayomilikiwa na Barrick Gold) kuwa Tanzania na si London nchini Uingereza wala Johannesburg, Afrika Kusini na jambo la saba, ni kazi za migodini sasa kufanywa na Watanzania.
Jambo la nane lenye manufaa kwa taifa katika maridhiano hayo, kwa mujibu wa Prof. Kabudi, ni kuwapo kwa mfuko maalumu wa kutafiti mchakato wa kujenga kiwanda cha uchenjuaji makinikia nchini; tisa ni wafanyakazi wa migodini sasa kupewa mikataba ya kudumu na si ya muda mfupi huku pia wakiishi na familia zao badala ya kuwapo katika kambi za migodi kama ilivyo sasa.
Aidha, jambo la 10 ni nafasi za juu muhimu za migodi kuwahusisha pia Watanzania; 11 ni Barrick kutojihusisha na madini mengine yanayopatikana (mbali na dhahabu, shaba na fedha), hivyo sasa metali mkakati zote kama lithium na rhodium zitakuwa ni mali ya serikali.
Jambo la 12 ni kesi na migogoro yote kimkataba kumalizwa na mahakama za Tanzania na siyo Ulaya ama kwingineko duniani huku pia, jambo la 13 lenye kuashiria ushindi kwa taifa ni Barrick kuilipa serikali dola za Marekani milioni 300 (takribani Sh. bilioni 700) huku majadiliano zaidi kuhusiana na madai ya kodi iliyolimbikizwa kwa muda mrefu yakiendelea baina ya pande mbili.
Aidha, jambo la 14 ni Barrick kuridhia masharti yote yaliyomo kwenye sheria mpya ya madini; jambo la 15 ni kila mgodi miongoni mwa mitatu inayomilikia na Barrick ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara kujitegemea katika uendeshaji na hivyo kulipa kodi kivyao; jambo la 16 ni Watanzania kuwa na uwakilishi katika bodi za migodi ya Barrick na hivyo kulinda maslahi ya taifa.
Katika makubaliano hayo, jambo la ushindi la 17 ni kuundwa kwa kampuni ya ubia wa usimamizi wa migodi ya madini iliyopo Tanzania ambayo itakuwa na makao makuu yake Mwanza na ofisi ndogo Dar es Salaam nchini Tanzania badala ya nchini Uingereza huku jambo la 18 likiwa ni kuimarisha huduma za jamii katika maeneo ya migodi kwa kuzingatia vipaumbele vya wananchi wenyewe wa maeneo husika.
Post A Comment: