KOCHA wa Azam FC, Zeben Hernandez amechekelea ratiba ya Kombe la Shirikisho barani Afrika na kudai kikosi chake kitafika mbali kwenye michuano hiyo.


Kauli ya Zeben imekuja baada ya kuona ratiba hiyo ambayo mashindano yake yanatarajia kuanza mwakani, na timu yake itaanza hatua ya kwanza kwa kucheza na mshindi wa jumla wa mechi ya raundi ya awali kati ya Orapa United ya Botswana na Mbabane Swallows ya Swaziland.

 Zeben alisema Azam FC wamejiwekea malengo ya kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo kutokana na usajili uliofanywa.

“Tumefurahi namna ratiba ilivyopangwa, tumeanzia raundi ya kwanza kutokana na ubora wa Azam FC tofauti na timu nyingine zinazoanzia raundi ya awali, kifupi tumepanga kufika hatua ya makundi, namna gani tutafikia ni kutokana na wachezaji waliosajiliwa kwani wana uzoefu,” alisema.

Zeben alisema ili kufika hatua ya makundi lazima kazi kubwa ifanyike na kila mtu kujituma kwenye nafasi yake na watajitahidi kujipanga kwa ajili ya mechi za michuano hiyo ikiwemo kuwafanyia tathmini wapinzani wao ambao wanatarajia kucheza naye.

“Naamini ni muda mzuri wa kujipanga zaidi kwani ni mashindano makubwa kinachotakiwa ni sisi kuingia tukiwa tayari ili ushiriki wetu uwe mzuri na kufika nafasi za juu zaidi,” alisema.

Azam FC itaanza kucheza ugenini na moja wa mshindi wa jumla wa mechi ya raundi ya awali kati ya Orapa United ya Botswana na Mbabane Swallows ya Swaziland Machi 10 hadi 12 mwakani kabla ya kurejeana nyumbani Azam Complex kati ya Machi 17 na 19.

Endapo watafuzu, wataingia raundi ya mwisho ya mtoano watakayocheza na moja ya timu 16 zilizotolewa kwenye raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikivuka itaingia moja kwa moja kwenye hatua ya makundi.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: