NG’OMBE 185 wamekufa kwa kipindi cha kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka huu katika ranchi ya Ruvu, mkoani Pwani kutokana na ukame.


Hayo yalisemwa na Meneja wa ranchi hiyo, Dk James Mtae wakati akitoa maelezo kwa Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba wakati alipofanya ziara katika eneo hilo kwa ajili ya kubaini changamoto mbalimbali zinazoikabili.

Akizungumzia ukame, Dk Mtae alisema mifugo hiyo ilikufa kutokana na kukosa majani katika eneo hilo. Alisema hata yale yaliyoletwa kutoka Kongwa mkoani Dodoma nayo yaliisha, hali iliyosababisha kuanza kudhoofika na hatimaye kufa.

“Njaa haiji kwa haraka, ni jambo ambalo huanza kidogokidogo lakini zipo jitihada mbalimbali ambazo zimefanywa katika kuokoa hali hiyo kutokea,” alisema Dk Mtae wakati akijibu kwa nini alisubiri hadi mifugo hiyo inadondoka bila kutafuta namna ya kuweza kuiokoa.

Alisema amejitahidi kwa kiwango cha kutosha, kwani ameweza kuisimamia mifugo hiyo kwa namna mbalimbali ili iweze kuishi, lakini kwa bahati mbaya na mabadiliko ya hali ya hewa, yaliyoleta ukame, ndio yaliyosababisha maafa hayo.

Hata hivyo, Waziri Tizeba alisema licha ya kuwepo kwa jitihada mbalimbali zilizofanyika, lakini kuna uzembe uliosababisha hali hiyo kutokea.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: