MWANASIASA Mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru, amesema bila ya kuwapo na Katiba mpya ni vigumu kwa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) na vingine vya upinzani nchini kuingia Ikulu.


Aidha, Kingunge aliyewahi kuwa kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka mingi na sasa kuonekana akiunga mkono misimamo inayoashiria mabadiliko, alisema wapinzani wasipopambana kuhakikisha katiba inaruhusu matokeo ya urais kuhojiwa mahakamani, ugumu huo wa kutimiza ndoto ya kuingia Ikulu utaendelea kuwapo katika kila uchaguzi. 

Ukawa huundwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chama cha Wananchi (CUF), NCCR-Mageuzi na NLD.

Kingunge aliyasema hayo jana wakati akizungumza katika mkutano na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, aliyekutana na wafuasi wa Chadema waliokuwa wanashikiliwa na Polisi kwa makosa mbalimbali ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana. 

Baadhi ya wafuasi hao ni wale wa kundi la ‘4U Movement’ na wengine waliokuwa wakikusanya matokeo ya uchaguzi ya mgombea wa Ukawa.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: