WATANZANIA wametakiwa kutoa taarifa wanabaini uwepo wa mchele usioeleweka, baada ya kuibuka kwa taarifa ya mchele bandia wa plastiki kukamatwa Nigeria.

Msemaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Gaudencia Simwanza alisema hayo jana .

Alisema wao sasa wana mifumo mizuri ya kudhibiti uingizwaji wa bidhaa zisizofaa na mpaka sasa mfumo huo haujabaini mchele wa aina hiyo nchini.

"Tunadhibiti na tuko makini kufuatilia wafanyabiashara wanaoingiza vitu haramu na kama huo mchele ungekuwa umeingia, tungeshajua," alisema.

Mwandishi wa habari hii alipomwuliza ikitokea umeingizwa kimagendo nchini, Watamzania watautambua vipi, Gaudencia aliwataka kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa watakapoona mchele wasiouelewa.

Mchele huo bandia ulikamatwa na Mamlaka ya Mji wa Lagos, Nigeria wiki hii, ambapo walikamata magunia 102.

Taarifa kutoka nchini humo, zilieleza kuwa uliingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu na unafanana na mchele wa kawaida, hivyo ni ngumu kuutofautisha na mchele wa kawaida.

Kutokana na kusambaa kwa kasi kwa mchele huo, huwezi kuutambua kwa haraka hadi pale unapopikwa ndipo unaweza kuona ni mchele wa plastiki. Hata hivyo baadhi ya wataalamu walisema kabla ya kuupika mchele huo ukilowekwa kwenye chombo chenye maji unaelea tofauti na halisi ambao huzama.
 
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: