ads

KWA mara ya kwanza tangu Tanganyika na Zanzibar kuungana ,kilele cha maadhimisho ya mwenge wa uhuru kwa mwaka huu zitaadhimishwa visiwani Zanzibar katika mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 14 mwezi huu.


Akizungumza na wanahabari hii leo ,Mkuu wa mkoa wa Mjini Magharib Mhe Ayoub Mohammed Mahmoud amesema kuwa mgeni rasmi katika siku hiyo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dk John Pombe Joseph Magufuli.

Aidha Mhe Ayoub amesema kuwa pamoja na tukio hilo ambalo limebeba kauli mbiu ya "Shiriki kukuza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya Uchumi" pia kutakuwa na matukio mengine muhimu ikiwemo kutamatisha wiki la vijana .

Mhe Ayoub amefafanua kuwa sherehe hizo zitakazofanyika katika uwanja wa Aman pia zitakuwa ni mahsusi kwa ajili ya kumbukizi ya kifo cha baba wa taifa Mwal Julius Kambarage Nyerere,ambapo zitaanza kwa ibada ya misa maalumu katika kanisa la Shangani posta .
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: