
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Jinsi ya kupika pilau ya kuku: Habari za leo wapenzi wasomaji wetu, Leo tunakuletea pishi la chakula kipendwacho na wengi, Pilau ya kuku. Fuatana nami hatua kwa hatua namna ya kupika wali huu.
Jinsi ya kupika pilau ya kuku: Hatua kwa hatua
Mahitaji
- Mchele wa basmati kilo 1
- Kuku ½
- Viazi 5
- Vitunguu 2
- Vitunguu Thomu(Saum) vilivyosagwa 3 vijiko vya supu
- Binzari ya pilau nzima 1 Kijiko cha chakula
- Binzari ya pilau 1 kijiko cha chai
- Pilipili manga nzima ½ kijiko cha chai
- Karafuu nzima 10
- Iliki nzima 8
- Mdalasini nzima 6 vijiti
- Pilipili mbichi iliyosagwa 3
- Chumvi kiasi
- Mafuta ya kupikia ¼ lita
Namna ya kupika pilau- Hatua kwa hatua
- Osha mchele na roweka kwa muda kutegemea na aina ya mchele.
- Kata kuku vipande upendavyo, safisha kisha chemsha vipande vyako pamoja na chumvi, pilipili iliyosagwa, thomu na tangawizi.
- Kuku akishawiva, mtoe weka kwenye bakuli safi, Bakisha supu katika sufuria.
- Tia mafuta kiasi katika sufuria, kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi na kuwa ya hudhurungi.
- Tia thomu na tangawizi na binzari zote, kisha kaanga tena kidogo.
- Tia viazi katika mchanganyiko wako huo, kisha endelea kukaanga kidogo.
- Tia vipande vyako vya kuku na supu (iliyobaki wakati wa kupika kuku) katika mchanganyiko wako huo, acha ichemke kidogo kisha tia maji, kisia kutokana na mchele unaotumia.
- Mwisho tia mchele koroga uchanganye na vitu vyote acha ichemke kiasi kisha funika na punguza moto mpaka uive (huku ukiugeuzageuza).
- Ukishakuwa tayari pakua kwenye sahani tayari kwa kula.
Pishi la pilau: Dondoo
Chakula hiki kinaweza kutosha mlo wa watu 3-4, unaweza kuongeza au
kupunguza vipimo vya mahitaji kulingana na idadi ya walaji. Pilau ya
kuku ni vizuri ikiliwa na salad na pilipili. Pia unaweza kushushia
pamoja na juisi ya matunda. Natumai umefurahia pishi letu la leo waweza
kutoa maoni yako hapo chini kuhusu jinsi ya kupika pilau ya kuku. Akhsanteni
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: