Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dkt. John Magufuli na mke wake Mama Janeth Magufuli leo wameshiriki Misa ya Krismasi katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatifu wa Yesu mkoani Singida. 


Rais amewahi kusali katika kanisa hilo kabla ya uchaguzi mkuu mwaka jana huku akimkumbuka Sister mmoja aliyemkabidhi rozali na kumuahidi kushinda nafasi ya urais katika uchaguzi huo.

Akizungumza katika ibada hiyo Rais Magufuli amesema rozali hiyo alikuwa anazunguka nayo kwenye ziara zake za kampeni hadi mwisho na kufanikiwa kupata kura za kutosha zilizompa ushindi.

Amesema kusali hapo ni moja ya sababu kubwa ya siri ya ushindi wake, na hivyo kuungana na wakazi wa mkoa wa Singida na watanzania wote kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo.

Magufuli ametumia fursa hiyo kuwataka watanzania kutumia Sikukuu ya Krisimasi kuimarisha upendo, kuvumiliana na kutobaguana, kwani njia ya upendo itasaidia taifa kujipatia maendeleo.

Aidha, amewataka wakulima kuhakikisha wanazitumia vizuri mvua za sasa katika kuchapa kazi ya kilimo kwa nguvu zote pamoja na kulima mazao yanayostahimili ukame.

Amesema Sikukuu ya Krismasi kunadhihirisha kauli mbiu ya 'hapa kazi tu', kwani Yesu Kristo alikuwa fundi mzuri wa useremala hivyo kuwataka watanzania kumuiga, na pia akiwataka wakazi wa mkoa wa Singida, kuongeza uzalishaji wa zao la alzeti ili kuviwezesha viwanda vya kukamua mafuta ya alzeti kupata mbegu nyingi.

Awali Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Singida, Edward Mapunda, amewakumbusha wakazi wa mkoa huo kuhakikisha wanatunza mazingira ili yaweze kuwatunza na kuwaepusha na ukame wa mvua.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: