
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
HALMASHAURI ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, imeanza msako wa
kuwatembelea walengwa wanaonufaika na Mfuko wa Jamii (TASAF) Awamu ya
Tatu.
Zaidi ya watu 80 wamekamatwa na kufikishwa mahabusu ya Kituo cha Polisi Bariadi kwa kudaiwa kufisadi fedha hizo.
Akizungumzia hilo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake jana,
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Abdallah Malela alisema kuwa jumla ya
kaya 80 katika halmashauri hiyo, zinatafutwa ili zirejeshe fedha zote.
Alisema imebainika kuwa kaya 80 ziliingizwa katika mradi wa TASAF III kwa njia za kinyemela na kuchukua Sh milioni 17.8.
“Ni kweli kuna msako huo, jumla ya kaya 80 hazikustahili kuwemo
katika mpango huu, tulifanya ukaguzi mpya baada ya maelekezo kutoka
Serikali Kuu kututaka kupitia upya walengwa, kama wanakidhi vigezo vya
kuwemo kwenye mpango,” alieleza Malela. Alisema kaya hizo zilibainika
kutokuwa na vigezo.
Ziliandikiwa barua tangu Agosti mwaka huu, kutaka warejeshe fedha
zote za miezi sita zilizotolewa kwao. Alieleza kuwa baada ya kupatiwa
barua hizo, hakuna kaya hata moja ambayo imeanza kurejesha fedha hizo.
Hali hiyo imesababisha kuwepo kwa msako huo wa nguvu. Alisisitiza kuwa wahusika hawatapewa dhamana mpaka warejeshe fedha zote.
“ Watu ambao tumewakamata hawapewi dhamana mpaka warejeshe fedha za
serikali. Mpaka leo tumefanikiwa kurejeshewa kiasi cha Shilingi milioni
1.1 kati ya milioni 17.8,” alieleza Malela.
Alisema msako huo utaendelea kwa halmashauri nzima mpaka pesa zote
zirejeshwe, ili kuweza kutumika kwa walengwa ambao walikusudiwa katika
mpango huo.
“ Leo ni siku ya tatu tunahangaika kupata dhamana, mama yetu
amekamatwa, wamesema ili kupata dhamana mpaka arejeshe kiasi chote
ambacho amepokea. Tangu aanze kuchukua fedha za TASAF anadaiwa shilingi
240,000,” alisema mmoja wa mtoto wa mnufaika, ambaye hakutaka kutaja
majina yake.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: