
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amewataka wazazi na walezi wa
visiwani Zanzibar, kuacha tabia ya kuwaoza wasichana wakiwa na umri
mdogo, bali wawasomeshe kwa ajili ya manufaa yao ya jamii kwa ujumla.
Samia alisema hayo kwa nyakati tofauti, wakati akizindua madarasa ya
kisasa iliyojengwa kwenye eneo la Kilimani na kukagua ujenzi wa vyumba
vya madarasa na ujenzi wa msikiti mkubwa kuliko yote nchini Tanzania
unaojengwa katika eneo la Ijitimai Kidoti mkoani Kaskazini Unguja.
Ujenzi huo unafanywa kwa michango ya wananchi. Alisema hayo katika siku yake ya kwanza ya ziara ya Kikazi Unguja.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais, Zanzibar, ilieleza kuwa makamu huyo wa Rais yupo katika ziara visiwani Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Samia alisema kama wazazi na walezi
watasomesha watoto wa kike, elimu watakayopata itasaidia kwa kiasi
kikubwa wasichana hao, kufanya maamuzi sahihi na yenye tija katika
jamii.
Alisisitiza kuwa elimu ni haki ya msingi kwa mtoto wa kike, hivyo ni
muhimu kwa jamii ya Zanzibar ihakikishe watoto wa kike wote wanapata
elimu, kwani watakuwa na uwezo wa kuchagua na kuandaa mustakbali wa
maisha yao ya baadaye, ikilinganishwa na hali ilivyo sasa kwenye baadhi
ya maeneo.
Kuhusu elimu ya dini, aliwahimiza wazazi na walezi, kuwalea watoto
katika maadili mema kwa kuzingatia maandiko matakatifu ya Mtume Mohammad
(S.A.W).
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: