Shirika la ugavi wa umeme nchini TANESCO limesema litafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha linarejesha hali ya upatikanaji wa umeme kwa baadhi ya maeneo jijini ambayo yamekumbwa na adha ya kukatika kwa umeme kutokana na kuharibika kwa Tranfoma 15mva iliyokuwa ikitoa huduma kwa wakazi wa wilaya ya Ilala.


Kauli hiyo ya kuwatoa hofu wananchi imetolewa na meneja wa TANESCO mkoa wa Ilala Mhandisi Atanasius Nangali wakati akiongea jijin Dar es Salaam ambapo amesema kukatika kwa umemem hivi karibuni katika baadhi ya maeneo kumetokana na hitilafu iliyotokea kwenye moja ya Tranfoma zinazo sambaza umeme huo ambapo wamefanya jithada ya kuwapatia umeme baadhi ya maeneo yalioathirika kutoka substation nyingine huku yakibaki maeneo matatu yamwanagati, Magole na baadhi ya maeneo ya kitunda.
 
Kutokana na kuongezeka kwa matumizi ya umeme hasa katika kipindi cha sikukuu  kaimu meneja uhusiano TANESCO Bi,Leila Muhija amewahakikishia wananchi upatikanaji wa umeme wa uhakika katika sikukuu pamoja na kuwataka wananchi kutosita kutoa taarifa za dharura ama hitilafu zinapojitokeza wakati wowote ili waweze kupata msaada wa haraka.
 
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: