
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
RAIS John Magufuli amekabidhi msaada wa vyakula mbalimbali na juisi
kwa kituo cha wazee wasiojiweza (SILABU) cha mjini Kigoma ikiwa ni kutoa
mkono wa sikukuu kwa watu wasiojiweza.
Msaada huo umekabidhiwa kwa wazee hao kwa niaba yake na Mkuu wa Mkoa Kigoma, Emmanuel Maganga.
Alisema msaada huo umetolewa kuwawezesha wazee hao kusherehekea sikukuu ya Krismasi sawa na watu wengine wenye uwezo.
Miongoni mwa vyakula vilivyokabidhiwa ni pamoja na kilo 90 za mchele,
mafuta ya kula ndoo tatu na mbuzi mmoja kwa ajili ya kitoweo.
Maganga naye alitoa katoni tano za juisi na miche 24 ya sabuni.
Mwenyekiti wa kambi hiyo, Hamisi Sabuni amemshukuru Rais Magufuli kwa
msaada huo, akisema tangu aingie madarakani ameonesha dhamira ya dhati
ya kuwajali watu wasiojiweza na wenye kipato duni.
Naye Ofisa Ustawi wa Jamii Mfawidhi wa Mkoa Kigoma, Heradius Mushi
alisema pamoja na serikali kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia chakula
kituoni hapo, bado kiasi cha fedha kinachotolewa hakikidhi mahitaji na
kuomba wahisani zaidi wajitokeze si tu nyakati za sikukuu, bali mara kwa
mara.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: