
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
KUNA mfumko mkubwa wa kilimo cha bangi nchini; na sasa baadhi ya watu
wanaendesha kilimo cha dawa hizo za kulevya kwa kutumia teknolojia ya
umwagiliaji.
Wengine wanalima bangi katikati ya hifadhi za misitu ya taifa na juu
ya milima, ambako ni vigumu kwa usafiri wa gari au pikipiki.
Wakati kilimo cha bangi kinashamiri, pia kumekuwepo na ongezeko la
watuhumiwa waliokamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na dawa zingine za
kulevya kama mirungi, kokeni na heroin. Ongezeko hilo linatokana na kazi
inayofanywa na kikosi kazi, kinachoundwa na taasisi mbalimbali
kuzidisha msako.
Kikosi kazi hicho kinaundwa na Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya,
Polisi, Uhamiaji, Mamlaka ya Mapato, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Jeshi
la Wananchi, Magereza na Takukuru.
Kikosi kazi hicho kinapambana na watuhumiwa wanaojihusisha na uingizaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya.
Akizungumza jana, Kamanda wa Kikosi cha Dawa za
Kulevya nchini, Mihayo Msikhela alisema mwaka huu zimekamatwa kilo
84.183.6 za dawa za kulevya, ukilinganisha na kilo 35,373 zilizokamatwa
mwaka jana. Idadi ya watuhumiwa pia imeongezeka kutoka 14,339 mwaka jana
hadi kufikia watuhumiwa 18,893 waliokamatwa mwaka huu.
Kilimo cha bangi Akizungumzia kilimo cha bangi, Msikhela alisema
kikosi kazi hicho, kimebaini kulimwa zao hilo kwa wingi katika safu za
milima mbalimbali nchini, ambako kutokana na jiografia ya huko ni vigumu
kufika kwa usafiri wa gari au pikipiki.
“Bangi ni janga la taifa, watu wamegeukia kilimo cha bangi na kuacha
kulima mazao mengine katika maeneo mengi nchini. Walimaji wanalima
katika maeneo ambako ni ngumu kuyafikia kwa usafiri wa magari au
pikipiki,” alisema Msikhela.
Alisema kutokana na msako mkali wa kikosi kazi hiyo, mwaka huu
kumekuwa na kesi nyingi na kiasi kikubwa cha bangi iliyokamatwa
ukilinganishwa na mwaka jana.
Alisema mwaka huu kumekuwa na kesi 8,159 zilizohusu bangi wakati
mwaka jana kulikuwa na kesi 6,752. Ongezeko la kesi za bangi ni 1,407.
Kiasi cha bangi ambacho kimekamawa mwaka huu ni kilo 65,804, tofauti na
mwaka jana ambako bangi iliyokamatwa ilikuwa ni kilo 20,066.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: