MSHAMBULIAJI wa Yanga, Donald amesema majukumu ya kiuchezaji aliyobadilishiwa na kocha George Lwandamina yamemfanya ashindwe kufunga na kazi hiyo amemwachia Amiss Tambwe.


Lwandamina amebadilisha mfumo wa uchezaji kati ya nyota hao wawili, ambapo sasa Tambwe ndiye atakuwa mfungaji huku Ngoma akipewa jukumu la kuwasaidia viungo kwa kutafuta mipira na kumtengenezea Tambwe.

Mzimbabwe huyo alisema kutokana na majukumu hayo yeye atakuwa akifunga mara chache sana, tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita, ambapo wote walikuwa wakicheza ndani ya eneo la hatari la timu pinzani na kila mmoja ana uhuru wa kufunga.

“Hizi ni mbinu mpya na unajua tumebadilisha kocha na kila mtu ana mbinu mpya, kwangu mimi nafurahia kwa sababu siyo mara ya kwanza kutumia mfumo huu, ingawa kitakachopungua ni kutofunga kama ilivyokuwa msimu uliopita na kwenye mzunguko wa kwanza,” alisema Ngoma.

Mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita aliifungia Yanga mabao 24, kwenye mashindano yote iliyoshiriki, alisema anaukubali sana uwezo wa Tambwe kwenye kufunga, hivyo hana wasiwasi, ispokuwa kazi kubwa anayo yeye na wachezaji wenzake kuhakikisha wanatengeneza nafasi nyingi za mabao.
 
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: