MBUNGE wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, ameahidi kupambana na ubadhirifu utakaojitokeza ndani ya jimbo lake.


Mbunge huyo pia amesema hayupo tayari kumvumilia mtendaji anayesababisha kero kwa wananchi badala ya kufanya jitihada ya kuzitatua.

Alitoa kauli hiyo juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kimara, Mtaa wa Mavurunza wilayani Ubungo.

Kubenea alisisitiza kuwa utendaji mbovu ni chanzo cha kuzorotesha maendeleo ndani ya jimbo.

Alisema kuwa lengo lao ni kuwapatia wananchi huduma muhimu ambazo ni haki yao kuzipata kama maji, barabara, shule, huduma za afya, soko na vituo vya polisi.

“Tutapambana na ufisadi na ubadhirifu wa namna yoyote utakaogundulika kufanywa na viongozi ndani ya eneo letu, sisi tumedhamiria kuleta mabadiliko na maendeleo kwa wananchi tunaowaongoza, hivyo hatupo tayari kumuacha mtu aharibu taswira yetu,” alisisitiza. 

Mbunge huyo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema kama kuna tatizo ndani ya uongozi kwenye kata, litatuliwa kwa njia ya vikao husika, hawataruhusu watu kuondoka madarakani bila kufuata utaratibu. 

Kubenea alisema tayari hatua za awali zimeanza kuchukuliwa kutatua suala la ukosefu wa maji, shule na barabara ikiwamo mazungumzo kuhusu ujenzi wa dharura wa shule ya sekondari ndani ya siku 90 ili kusajili wanafunzi wenye uwezo ambao walikosa nafasi ya kuendelea na masomo.

“Watoto 859 wamefaulu kujiunga na masomo ya sekondari, lakini 492 tu ndiyo wamepangiwa shule…kwa sasa tunahitaji madarasa manane ili kuwezesha idadi hiyo ya wanafunzi kuanza masomo,” alisema.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: