KOCHA wa Yanga, Mzambia George Lwandamina amepingana na maoni kwamba Yanga imepangwa na vibonde katika Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.


Mabingwa wa Tanzania, Yanga wataanza na Ngaya de Mbe ya Comoro na Lwandamina amesema hiyo si timu ya kubeza kwa kuwa ratiba nzima ya raundi ya awali imehusisha timu zenye viwango sawa.

“Droo iko sawa, wapinzani wetu si timu ya kubeza natarajia ushindani na tutahitaji maandalizi mazuri kabla ya mchezo huo,”alisema.

Yanga wataanzia ugenini wikiendi ya Februari 10 hadi 12 kabla ya marudiano wikiendi ya Februari 17 hadi 19, mwaka huu na wakivuka hatua hiyo watakutana na mshindi kati ya Zanaco ya Zambia na APR ya Rwanda katika Raundi ya kwanza wakianzia nyumbani Machi 10 hadi 12 kabla ya marudiano Machi 17 hadi 19 mwakani, 2017.

Lakini Lwandamina amesema hawezi kuzungumzia hatua inayofuata kukutana na mshindi kati ya Zanaco na APR kabla ya kuvuka mtihani uliopo mbele yake dhidi ya mabingwa Comoro.

“Siwezi kuzungumzia mechi hiyo, subiri wakati wake utakapofika ndipo nitaizungumzia kwa sasa tunaelekeza nguvu zetu kwenye mtihani uliopo mbele yetu,”alisema.

Lwandamina aliyejiunga na Yanga mapema Novemba, anakabiliwa na changamoto ya kuipiku rekodi ya mtangulizi wake, Mholanzi Hans van der Pluijm ambaye mwaka huu aliifikisha Yanga hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutulewa na Al Ahly ya Misri.

Yanga ikaangukia kwenye kapu la kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, ambako ilifanikiwa kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola na kuingia Kundi A pamoja na TP Mazembe ya DRC, MO Bejaia ya Algeria na Medeama SC ya Ghana.

DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA  

ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: