
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi π΅πͺπ΅πͺ
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako
amewataka wadau wa elimu mkoa wa Mbeya kujitafakari baada ya Mkoa huo
kufanya vibaya katika matokeo ya mtihani wa darasa saba mwaka huu.
Profesa Ndalichako ametoa agizo hilo kwenye Mahafali ya Pili ya
Mafunzo ya Uongozi na Usimamizi Elimu ya Chuo cha Wakala wa Maendeleo ya
Utawala wa Elimu(ADEM) yaliyofanyika jijini Mbeya.
Amesema mkoa wa Mbeya umekuwa wa 22 kati ya mikoa 26 hivyo
kudhihirisha kuwa ulifanya vibaya na ni lazima kila mdau ajitafakari ni
kwa namna gani amechangia matokeo hayo mabaya.
Ameagiza uongozi ngazi ya mkoa na halmashauri kuhakikisha unajipanga
kutumia fursa zilizopo ili kuondokana na aibu kwa kufanya vizuri kwenye
mitihani ya kitaifa.
Amewataka pia walimu wakuu kuhakikisha wanakuwa wasimamizi wa kwanza
wa raslimali za shule sambamba na kusimamia viwango bora vya taaluma.
Wahitimu wa mafunzo hayo ya mwaka mmoja ambao wote ni walimu wakuu
kutoka shule za mikoa ya Mbeya, Songwe, Njombe na Iringa, waliiomba
Serikali kuendeleza kozi hiyo wakisema imewajengea uwezo zaidi wa
kiutawala.
Mwalimu Josephat Mahimbi akisoma risala alisema, awali walimu wakuu
walikuwa na wakati mgumu kiutendaji kwa kuwa walikuwa wakiteuliwa
kushika nyadhifa hizo pasipo kuwa na muongozo wowote.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
ANDIKA MAONI YAKO HAPO CHINI
Post A Comment: